Akasema: “Kunaushirikiano mkubwa baina ya Ataba katika kuhudumia mazuwaru, ushirikiano huu unatokana na Atabatu Abbasiyya namna inavyojitolea katika kuhudumia mazuwaru wanaokuja kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kuna huduma tofauti zinazotolewa na maukibu ya Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru katika mji wa Kadhimiyya, zimesaidia kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa na Atabatu Kadhimiyya na kupata mafanikio makubwa”.
Mwisho akatoa shukrani kwa Atabatu Abbasiyya kutokana na namna inavyo saidia Ataba zingine katika kuhudumia mazuwaru kwenye matukio tofauti yanayohusu Ahlulbait (a.s).