Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya semina ya kidini ya kwanza katika jimbo la Panjab nchini Pakistani.
Semina hiyo imesimamiwa na Maahadi ya turathi za Mitume tawi la Urdu chini ya kitengo.
semina zimefanywa kwenye vitongoji thelathini na kuhudhuriwa na zaidi ya wanafunzi (200) na imedumu kwa muda wa siku (25).
Masomo yaliyofundishwa ni Fiqhi kwa mujibu wa Mheshimiwa Sayyid Ali Sistani, Aqida, Akhlaq, Sira na hukumu za usomaji wa Qur’ani.
Maahadi inalenga kusambaza utamaduni wa kiislamu na kujenga uwelewa kwa vijana, sambamba na kuwafundisha hukumu za Dini na mambo muhimu katika Maisha yao.
Maahadi imekusudia kufanya Semina nyingine baada ya Idul-Adh-ha, kwenye kitongoji cha Sayalikut katika jimbo la Pamjab.