Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya hafla ya (mimbari za nuru) kwa ushiriki wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa.
Hafla hiyo ni sehemu ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa unaosimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Mimbari ya hafla hiyo imepandwa na msomaji Mauhubu Ibrahim Abdullahi mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, akafuata Shekhe Ali Saidi na mwisho akasoma Muhammad Abdushahidi na muendesha hafla alikuwa ni Sayyid Hasanaini Jazaairi.
Hafla imepata muitikio mkubwa wa wadau wa Qur’ani tukufu, wahudhuriaji wamesikia visomo tofauti kutoka kwa wanafunzi wa mradi na walimu wao.
Hafla imerushwa moja kwa moja na chanel ya Qur’ani kutoka kwenye luninga ya Karbala.