Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza umuhimu wa kujenga mahusiano baina ya raia na kuimarisha umoja wa kitaifa.
Ameyasema hayo wakati akipokea vijana wenye asili ya Iraq wanaoishi Ulaya katika chuo kikuu cha Alkafeel mjini Najafu.
Ziara ya wageni hao imeratibiwa na kituo cha kiiraq cha kuthibitisha jinai za magaidi, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya.
Sayyid Swafi ameonyesha umuhimu wa ziara hii, katika kujenga ushirikiano baina ya raia wa Iraq na kuimarisha umoja wa kitaifa, sambamba na kuonyesha picha nzuri ya wananchi wa Iraq kwenye mataifa wanayoishi.
Mheshimiwa amehimiza kuondoa picha ya mauwaji na ugaidi waliyonayo mataifa mengine dhidi ya taifa la Iraq kwa sababu ya yaliyotokea miaka ya nyuma, akatoa wito wa kuwa na hutuba za uadilifu na zinazohimiza kusameheana.
Wageni wamepongeza kazi kubwa inayofanywa na Atabatu Abbasiyya hapa nchini, wakasema kuwa Ataba imekuwa fahari kubwa kwa wairaq wanaoishi Ulaya, aidha wameshukuru mapokezi mazuri waliyopewa na wakaomba Ataba iendelee kuwajali na kuwaalika raia wa Iraq wanaoishi katika nchi za kigeni.