Ujumbe kutoka Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, umetembelea semina za Qur’ani katika mkoa wa Misaan.
Ratiba ya kutembelea semina za Qur’ani inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu chini ya Majmaa.
Mjumbe wa harakati za Qur’ani katika Maahadi Sayyid Hussein Habubi amesema “Semina za Qur’ani zinazoendelea zinaushiriki wa wanafunzi (5150), zinafanywa kwenye misikiti na huseiniyya (130) na kuna jumla ya walimu (150)” akabainisha kuwa “Kuna fomu maalum inayozingatia vigezo vya kimataifa vya kuwapima walimu na semina kwa lengo la kuwaendeleza zaidi”.
Akaongeza kuwa “Ziara ya wageni hao imefanywa kwa kushirikiana na muwakilishi wa Marjaa Dini, sehemu walizotembelea ni, wilaya ya Al-Azizi, Qal’atu-Swalehe, mtaa wa Al-Adl, Alkhair na wilaya ya Majrul-Kabiir, inahusisha makao makuu ya mkoa, wilaya ya Kumiyat, magharibi na mashariki ya Kahlaai na Musharaha, Maimuna na mtaa wa Salaam”.
Majmaa-Ilmi inafanya ziara endelevu kwa ajili ya kubaini mahitaji muhimu na kuangalia mwenendo wa masomo, sambamba na kusikiliza maoni ya walimu na ziongozi kwa lengo la kuweka mazingira bora kwa walimu na wanafunzi.