Idara ya wahadhiri tawi la wanawake imeadhimisha kumbukumbu ya ndoa ya nuru mbili (a.s).

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeadhimisha kumbukumbu ya ndoa ya kiongozi wa waumini Imamu Ali na bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Hafla imefanywa katika kituo cha Swidiqah-Twahirah (a.s) kwa kushirikiana na watumishi wa kituo hicho, hafla imepambwa na tenzi za kuwasifu Ahlulbait (a.s) na khutuba ya kueleza utukufu wa Imamu Ali na bibi Zahara (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu.

Katika hafla hiyo yamefanywa mashindano ambayo wahudhuriaji wameshiriki, ikahitimishwa kwa kusoma Duaau-Faraji ya kuomba kudhihiri haraka kwa Imamu Mahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: