Kitengo cha usimamizi wa haram kimeanza kufanya maandalizi maalum ya ziara ya Arafa.

Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kimeanza kufanya maandalizi ya kupokea mazuwaru watakaokuja kufanya ziara ya Arafa.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema kuwa, kitengo kimeanza kufanya maandalizi maalum ya ziara tukufu ya Arafa, tunaweka vizuwizi vya kuongoza matembezi ya mazuwaru sambamba na kutandika mazulia.

Akaongeza kuwa, “Tumeweka vizuwizi vya mbao karibu na milango ya Sardabu kwa ajili ya kuongoza matembezi ya mamilioni ya mazuwaru, ili kurahisisha uingiaji ndani ya haram na kwenye sardabu bila msongamano wowote”.

Zimeandaliwa sehemu maalum za kupita mazuwaru bila kusababisha msongamano wowote kwa mazuwaru na kuhakikisha wanafanya ziara kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: