Mpiga picha wa kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya bwana Liith Ahmadi Haadi, amekuwa mshindi wa pili kwenye shindano la kimataifa ya upigaji wa picha lililopewa jina la “Matembezi ya wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) katika ziara ya Arubaini”.
Picha ya Haadi imepata nafasi ya pili kwenye shindano lililoandaliwa na taasisi ya Naharaini ya vijana na maendeleo endelevu, katika jumla ya picha (1275) zilizoshiriki.
Picha zilizopita kwenye mchujo zilikuwa (368) kutoka nchi (20) za kiarabu na kiajemi.
Haadi ameushukuru uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na idara ya kitengo cha Habari kwa ushirikiano mkubwa aliopata.