Kitengo cha utumishi kimeandaa zaidi ya sehemu (10) za kutunzia vitu vya mazuwaru.

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kimeandaa sehemu zaidi ya (10) kwa ajili ya kuntunzia viatu vya mazuwaru katika maeneo yanayozunguka jengo la Ataba tukufu.

Maeneo hayo yanasimamiwa na idara ya viatu chini ya kitengo hicho.

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Abbasi Ali amesema “Kitengo hutoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa lengo la kurahisisha utendaji wao wa ibada ya ziara, na moja ya huduma hizo ni hii inayofanywa na idara ya viatu”.

Akaongeza kuwa “Idara inasimamia sehemu zaidi ya kumi za kutunza viatu na mali za mazuwaru, zipo sehemu za wanaume na wanawake”. Akafafanua kuwa “Wanaume wanasehu maalum miongoni mwake ni mlango wa Qibla, mlango wa Hassan (a.s), Mlango wa mkono na mingineyo, aidha kuna milango maalum kwa ajili ya wanawake pia, kazi ya kutunza viatu na mali za mazuwaru hufanywa kila siku saa zote”.

Wahudumu wa kitengo cha Utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara zao zofauti wanatoa huduma kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala kwa muda wa saa (24) kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: