Rais wa kiengo cha kudhibiti ubora katika chuo hicho Dokta Muhammad Rafii amesema “Mfumo wa (Round University Ranking) ni moja ya mifumo ya kulingalisha ubora wa vyuo na maahadi kielimu duniani”.
Akaongeza kuwa “Chuo kikuu cha Alkafeel kimekuwa chuo cha (1195) kimataifa na cha (31) kitaifa, na cha (15) katika vyuo binafsi kwa mwaka wa masomo wa (2023m)”.
Akabainisha kuwa “Chuo kimekuwa kikifanyia kazi mfumo wa kuboresha elimu kwa kupeleka walimu wake kufanya tafiti na kuandiaka Makala za kimataifa na kitaifa”.