Wanafunzi (1000) katika wilaya ya Madaaini mkoani Bagdadi wamejiunga na mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi.

Wanafunzi zaidi ya (1000) katika wilaya ya Madaaini mkoani Bagdad wamejiunga na mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi zinazo simamiwa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya.

Majmaa inaendelea kutoa huduma za Qur’ani kwa raia wa mji mkuu wa Bagdad, kwa kufundisha usomaji wa Qur’ani tukufu na kuihifadhisha, Pamoja na masomo ya Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira.

Mradi unalenga kujenga uwelewa wa utamaduni na Qur’ani kwa vijana na kutumia vizuri kipindi cha likizo ya majira ya kiangazi.

Wanafunzi wanashiriki kwenye semina hizi kutoka vitongoji vyote vya mji mkuu wa Bagdad wanazidi (1000), wapo katika misikiti na Husseiniyya zaidi ya (200) na kuna walimu zaidi ya (360).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: