Mbele ya katibu mkuu.. Atabatu Abbasiyya yatoa zawadi kwa wastafu wake.

Atabatu Abbasiyya imewapa zawadi wastafu wake mbele ya katibu mkuu Sayyid Mustwafa Aalu Dhiyaau-Dini siku ya Ijumaa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, pamoja na marais wa vitengo na kundi la wastafu.

Mheshimiwa katibu mkuu amesema “Atabatu Abbasiyya imefanya kikao maalum cha kuwazawadia wastafu ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), kama sehemu ya kuthamini mguvu yao waliyojitolea wakati wote wa utumishi wao katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”, akasisitiza kuwa “Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi anafikiri kutoa kitu kwa wastafu na familia zao, ikiwa ni pamoja na kuwapa makazi na posho ya kila mwezi kwa ajili ya kujikimu”.

Akaongeza kuwa “Kikao hiki ni ujumbe tosha kwa watumishi wetu, hakika siku za utumishi katika malalo ya mwezi wa familia huisha na mtu hufika umri wa kustafu, jambo hili linatukumbusha kufanya kazi kwa bidii na kutumia vizuri muda ambao tumewafikiwa kuwa jirani na malalo takatifu na kuhudumia mazuwaru”.

Wastafu wamefurahi kuandikwa majina yao kwenye orodha ya wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wakashukuru Atabatu Abbasiyya kwa kuwapa zawadi na kuonyesha thamani ya utumishi wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: