Sayyid Swafi: Amewaambia watu wa wilaya ya Alkuful.. Hifadhini mazao yenu ya kilimo hakika ni sehemu ya utambulisho wenu.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amewaambia watu wa wilaya ya Alkuful katika mkoa wa Baabil kuhusu kuhifadhi mazao yao ya kilimo, kwani ni sehemu ya utambulisho wa wilaya hiyo kihistoria.

Ameyasema hayo alipokutana na ujumbe kutoka wilaya ya Alkuful mkoani Baabil.

Mheshimiwa Sayyid Swafi amewaambia kuhusu huduma zinazotolewa na Atabatu Abbasiyya katika wilaya hiyo, sambamba na changamoto wanazopata watu wa mji huo.

Akaeleza umuhimu wa malalo nyingi za kidini za watoto wa Maimamu zilizopo katika mji huo, ambapo wanaweza kutumia kujenga misingi ya utamaduni na Dini katika eneo hilo, sambamba na kuangalia namna ya kuchangia maendeleo ya wilaya katika sekta tofauti.

Akasisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazao ya kilimo, kwani ni sehemu ya utambulisho wa wilaya hiyo, akasema kuwa shirika la Khairul-Juud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lipo tayali kutoa msaada wa kutibu maradhi yanayoipata baadhi ya miti katika mji huo.

Mheshimiwa Sayyid Swafi akatoa wito kwa watu wa wilaya ya Alkuful wa kutembelea Atabatu Abbasiyya na kuangalia miradi yake, pamoja na kushiriki kwenye mprogram za kitamaduni, akasema kuwa milango ya Atabatu Abbasiyya iko wazi kwa wakazi wa wilaya ya Alkuful.

Kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya akahimiza kuwajali vijana, na kuwajenga katika misingi ya Dini yao sambamba na kuinua vipaji vyao na ubunifu wao.

Aidha Mheshimiwa Sayyid Swafi amehimiza kuenzi utamaduni, hususan ule unaotambulisha taifa na nafasi ya viongozi wa koo na kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: