Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kuondoa uvimbe kwenye nyonga ya kushoto ya mgonjwa mwenye umri wa zaidi ya miaka 20.
Daktari bingwa wa mifupa katika hospitali hiyo Dokta Mustwafa Walidi amesema: “Mgonjwa mwenye umri wa miaka (23) alikua na tatizo la maumivu ya nyonga, baada ya kumfanyia vipimo tukagundua tatizo hilo limeathiri hadi sehemu ya kibofu”.
Akafafanua kuwa “Tumemfanyia upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu, tumeondoa uvimbe wote kwenye nyonga na tumepandikiza mfupa upande wa nyonga ya kushoto”, akabainisha kuwa “Mfupa tuliopandikiza sehemu ya mfupa huo ni wa kutengenezwa na sehemu nyingine imetokana na mfupa halisi tuliochukua kwenye muili wake mwenyewe”.