Mawakibu za uombolezaji katika mji wa Karbala kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, hufanya uombolezaji katika tarehe za kumbukumbu za vifo vya watu wa nyumba ya Mtume (a.s).
Sayyid Faaiq Hussein amesema “Kikundi cha vijana wa Zainabiyya na mawakibu za kuomboleza, wameomboleza kifo cha Imamu Baaqir (a.s)”. akabainisha kuwa “Mawakibu zinaendelea kuja kutoa pole kufuatia kumbukumbu ya msiba huo mkubwa kwa Ahlulbait (a.s)”.
Naye Sayyid Fadhil Abbasi kutoka maukibu ya watu wa Karbala amesema “Matembezi ya kuomboleza ni desturi ya watu wa Karbala waliyorithi kutoka kwa babu zao, kila tarehe ya kumbukumbu ya kifo cha Imamu miongoni mwa maimamu wa Ahlulbait (a.s), huja kutoa pole kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.