Wahudumu wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Imamu Baarir (a.s).

Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wameomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.

Maukibu imefanya matembezi kuanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili huku wanaimba qaswida za kuomboleza zilizo ibua hisia za majonzi na huzuni katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Baada ya kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wamefanya majlisi ya kuomboleza iliyohudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru, qaswida na tenzi mbalimbali za kuomboleza zimesomwa kwenye majlisi hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: