Maukibu ya watu wa Karbala inaomboleza kifo cha Muslim bun Aqiil katika msikiti wa Kufa.

Maukibu ya watu wa Karbala imeomboleza kifo cha balozi wa Imamu Hussein (a.s) Muslim bun Aqiil kwenye msikiti wa Kufa katika mkoa wa Najafu.

Makamo rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Hashim Mussawi amesema kuwa “Watu wa Karbala wamesanyika katika maukibu moja na wanashirikiana na kitengo cha maadhimisho kayika kuomboleza kifo cha balozi wa Imamu Hussein (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Baada ya kuwasiri katika msikiti wa Kufa mjini Najafu imefanya majlisi ya kuomboleza iliyo hudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru, na kusomwa qaswida na tenzi nyingi za Husseiniyya”.

Akaendelea kusema “Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeandaa usafiri wa kubeba watu kutoka Karbala hadi msikiti wa Kufa pamoja na huduma zingine za kibinaadamu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: