Majmaa-Ilimu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir na Muslim bun Aqiil (a.s).

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir na Muslim bun Aqiil (a.s) kwa wanafunzi wa semina za Qur’ani katika mji wa Kirkuuk.

Majlisi imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Najafu chini ya Majmaa.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyofuatiwa na muhadhara kuhusu historia ya Imamu Baaqir (a.s), na kupata mazingatio kutoka katika Maisha yeke matukufu.

Majmaa inafanya makumi ya majlisi za kuomboleza katika mikoa yote zinakofanyika semina za majira ya kiangazi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: