Shirika la Alkafeel la maji safi limesema: Tumeandaa deli 150,000 kwa ajili ya kuwekea maji safi ya kunywa mazuwaru wa siku ya Arafa.

Shirika la Alkafeel la maji safi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limesema kuwa limeandaa deli laki moja na elfu hamsimi (150,000) kwa ajili ya kuwekea maji ya kunywa mazuwaru wa siku ya Arafa.

Mkuu wa kamati ya utendaji Sayyid Qahtwani Jayadi Abudi amesema “Wahudumu wa kitengo chetu huandaa mamia ya deli za maji kulingana na wingi wa mazuwaru, hususan wakati kama huu wenye joto kali”.

Akaongeza kuwa “Uandaaji wa deli hizo ni sehemu ya maandalizi kamili ya ziara ya mwaka huu” akabainisha kuwa “Tumeandaa deli (150,000) pamoja na barafu za kutosha kwa ajili ya mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Idara yetu huwajibika kuandaa maji safi ya kunywa kwa ajili ya mazuwaru wanaokuja katika mkoa mtukufu wa Karbala na kugawa kwa Mawakibu Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: