Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s).
Kiongozi wa Idara bibi Taghrida Tamimi amesema “Idara yetu imeomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) kwa kufanya majlisi ya uombolezaji na wanafunzi wa semina za majira ya kiangazi ndani ya kumbi wa shule za Al-Ameed”.
Akaongeza kuwa “Idara inafanya juhudi ya kueneza utamaduni wa Ahlulbait (a.s) na kulea vizazi katika mwenendo wao”, akabainisha kuwa “Kufanya majlisi za Husseiniyya ni jambo muhimu kwa ajili ya kufundisha mwenendo wa Maimamu (a.s)”.
Akasema kuwa “Majlisi ilihitimishwa kwa kusoma qaswida za kuomboleza na Duaau-Faraji ya Imamu wa zama (a.f)”.