Maandalizi ya siku ya Arafa.. wataalamu wa Alkafeel wamemaliza mazowezi ya uokozi kwa kikosi cha utoaji wa huduma ya awali.

Wataalamu wa Alkafeel kitengo cha mafunzo ya uokozi katika Atabatu Abbasiyya, wamekamilisha mafunzo kwa kikosi cha madaktari wa Atabatu Abbasiyya kwa ajli ya kujiandaa na ziara ya siku ya Arafa na Idul-Adh-ha.

Kiongozi wa huduma za kidaktari Sayyid Akram Hussein Al-Atabi amesema “Miongoni mwa ratiba ya program ya uokozi na huduma za kidaktari, ni kuandaa kikosi maalum kwa ajili ya kutoa huduma hizo kwenye ziara zinazohudhuriwa na mamilioni ya watu, kama vile ziara ya siku ya Arafa na Idul-Adh-ha”.

Akaongeza kuwa “Baadhi ya wahudumu wa Ataba kutoka vitengo tofauti wameshiriki kwenye mafunzo ya uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza”.

Kesho watawekwa kwenye maeneo maalum kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru watukufu, miongoni mwa maeneo hayo ni, uwanja wa katikati ya haram mbili, kwenye milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu, Barabara ya Ta-Amiin na barabara ya Abbasi (a.s), watakuwa tayali kutoa huduma ya uokozi na kidaktari kwa haraka wakati wowote itakapohitajika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: