Maelfu ya waumini wamefanya ibada maalum za siku ya Arafa mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Watu wamekuja kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kufanya ibada maalum ya siku hii tukufu mbele ya malalo takatifu, huku ulinzi na usalama ukiwa umeimarishwa.
Maelfu ya watu wanaume kwa wanawake wamefanya ziara, kusoma dua, kuswali na ibada zingine mbalimbali chini ya jua, kwani uwanja wa katikati ya haram mbili na marabara zinazo zunguka haram pamoja na sehemu zote za pembezoni mwa haram zimejaa mazuwaru waliokaa kila sehemu wakifanya ibada.
Kawaida waumini kutoka kila mahala huja kufanya ibada za mwezi tisa Dhulhija mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), vitengo vya Ataba hujiandaa vizuri na kutoa huduma mbalimbali kwa waumini hao.