Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na wajumbe wa kamati kuu pamoja na marais wa vitengo, wameshiriki katika kupokea wageni na salam za Idi.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Karbala wamekuja Atabatu Abbasiyya kutoa salam za Idhul-Adha-ha.
Katika kubadilishana salam za Idi wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu, arudishe tukio hili mwakani huku taifa likiwa na amani na utulivu.