Shekhe Karbalai amefuatana na idadi kubwa ya viongozi kutoka Atabatu Husseiniyya waliokuja kutoa pongezi kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ugeni huo umepokelewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.
Wamepeana salamu za Idul-Adha-ha na kumuomba Mwenyezi Mungu arudishe tukio hili kwa taifa letu likiwa na amani.
Ataba imepokea mashekhe mbalimbali wa mkoa wa Karbala, viongozi wa ngazi tofauti na watu wa kawaida, bila kusahau maelfu ya mazuwaru walikuja kutoa salam za Idi.