Kwa picha.. Mazingira ya ziara ya siku ya kwanza katika Idul-Adh-ha ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya nchi katika siku ya kwanza ya Idhul-Adha-ha waliokuja kufanya ibada ya ziara.

Asubuhi ya Alkhamisi mazuwaru wameswali swala ya Idi ndani ya haram takatifu, Atabatu Abbasiyya imefanya maandalizi mazuri ya kupokea mazuwaru kutoka kila mahala pamoja na wanaokuja kutoka nchi zingine, matembezi yao yamesimamiwa na kupangiliwa vizuri.

Waumini wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alitunuku amani taifa la Iraq na awarehemu mashahidi wa Iraq na kuwaponya haraka majeruhi.

Katika siku ya kwanza ya sikukuu hii tukufu mazingira ya shangwe na furaha umeenea katika haram za malalo mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: