Kitengo cha maarifa kinafanya semina kuhusu uhakiki wa nakala-kale.

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimefanya semina iliyopewa jina la “Nafasi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika uhakiki wa nakala-kale”.

Semina imesimamiwa na idara ya kusimamia elimu, nayo ni sehemu ya kuboresha uwezo wa vijana katika sekta ya uhakiki na kutengeneza kizazi kipya cha wahakiki.

Muwezeshaji wa semina hiyo alikuwa ni Shekhe Muhammad Dhwalimi, imehudhuriwa na wanafunzi (22) waliokuja Karbala kusoma Dini kutoka ndani na nje ya Iraq.

Semina imedumu kwa muda wa siku kumi na mbili, ilikuwa na mihadhara (26) kila siku mihadhara miwili, wamefundishwa masomo ya nadhariyya na misingi ya uhakiki.

Semina imehitimishwa kwa kufanya mtihani wa kielimu na kubaini waliofanya vizuri katika washiriki, ambao wataingizwa katika hatua ya pili na kuwapa nafasi ya kufanya uhakiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: