Idara inayosimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa ziara ya siku ya Arafa na Idul-Ahd-ha.
Kiongozi wa idara Sayyid Aqiil Twaifu amesema “Wahudumu wa idara wamepata mafanikio makubwa katika kutekeleza mkakati wa ziara ya siku ya Arafa na Idul-Adh-ha” akabainisha kuwa “Matembezi ya mazuwaru yamefanyika vizuri bila kuwepo msongamano wowote”.
Akaongeza kuwa “Tuliweka vizuwizi baina ya wanawake na wanaume ndani ya haram tukufu, sardabu ziliendelea kupokea mazuwaru wa kike kwa mistari iliyo simamiwa vizuri jambo lililowezesha mazuwaru kushika kaburi bila msongamano”.
Akaendelea kusema “Mlango wa Alqami uliwekwa maalum kwa ajili ya kuingia watu wanaotumia viti mwendo na mikokoteni, sambamba na kuratibu matembezi ya ndani ya haram na sehemu za kuswalia, kulikuwa na sehemu maalum za kuingia na kutoka mazuwaru zilizo andaliwa kwa kushirikiana na vitengo vingine”.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara, wahudumu wa idara hii huwajibika kuweka vitabu vya dua na ziara kwenye kabati za vitabu, sambamba na kuokota mali zilizopotea na kuzipeleka kwenye idara husika, bila kusahau kazi ya kufanya usafi na kupuliza marashi wakati wote.