Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya imeandaa program ya mapumziko kwa wanafunzi wa mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi.
Mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi unasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu.
Program inahusisha kufanya maigizo, kutembelea sehemu mbalimbali, michezo na mambo mengine yanayojenga furaha kwa wanafunzi, yote hayo yatafanywa chini ya wakufunzi mahiri.
Kupitia mazowezi na michezo, Jumuiya inalenga kuimarisha afya za wanafunzi na uwezo wa kiakili sambamba na kuboresha vipaji vyao, ili waendelee kuhifadhi Qur’ani tukufu kwa urahisi.