Wanafunzi elfu nane wanaendelea kupata masomo ya Dini kwenye mradi wa semina za Qur’ani katika mji wa Najafu.

Wanafunzi wa mradi wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi kwenye mji wa Najafu wanafundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu, Fiqhi na Aqida.

Kuna zaidi ya wanafunzi (8000) wanaoshiriki kwenye semina, miongoni mwa masomo wanayofundishwa ni Fiqhi, Qur’ani, Aqida, Akhlaq na historia za Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kuwajenga kidini na kijamii pamoja na kuwafundisha mwenendo wa Ahlulbait (a.s).

Ugeni kutoka Maahadi ya Qur’ani tukufu, umetembelea vituo vinavyo tumika kuendesha semina hizo, na kuangalia mambo yanayohitajika katika kufanikisha zowezi hilo.

Semina za Qur’ani tukufu za majira ya kiangazi zinazosimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa Ilmi ya Qur’ani tukufu, zilianza mwezi uliopita katika mikoa tofauti huku kikiwa na washiriki zaidi ya elfu (54), na idadi kubwa ya walimu wa Qur’ani tukufu walio andaliwa rasmi kwa ajili ya semina hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: