Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya, kinafanya semina ya pili kwa walimu ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo.
Kiongozi wa idara ya mafunzo Sayyid Farasi Shimri amesema “Tumeanza kutoa mafunzo maalum kwa watumishi wa Ataba tukufu, kwa lengo la kuboresha uwezo wa walimu”.
Akaongeza kuwa “Siku ya kwanza mtoa mada alikuwa ni Sayyid Ali Shimri, ameongea kuhusu umuhimu wa mafunzo na faida za semina”.
Akasema kuwa “Mwisho wa semina kutakuwa na maonyesho ya kielimu, yatakayo fanywa na washiriki wa semina, semina itadumu kwa muda wa siku kumi na kila siku ina saa saba za masomo”.