Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imeanza muhula wa pili wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa awamu ya saba.
Harakati hiyo inasimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Mkuu wa kamati ya utendaji Sayyid Muhammad Ridhwa Zubaidi amesema “Muhula wa pili wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa awamu ya saba utadumu kwa muda wa siku kumi na tano”.
Akaongeza kuwa “Awamu ya pili itakuwa na ratiba ya masomo ya kidini, kitamaduni na burudani, sambamba na kuendeleza masomo ya mbinu za kuhifadhi Qur’ani”.
Akaendelea kusema “Mradi unalenga kuibua vipaji vya usomaji wa Qur’ani kwa vijana wenye umri wa miaka (18) na chini ya hapa, awamu hii inawashiriki zaidi ya (100)”.