Kiongozi wa moja ya sehemu za ukanda huo Sayyid Amiin Arkani Ahmadi amesema “Kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, mradi wa ukanda wa kijani unaendelea kukaribisha familia za watu wanaopenda kuja kutembelea mandhari za ukanda huu katika siku za Idul-Adh-ha tukufu”.
Akaongeza kuwa “Tumeandaa mazingira mazuri ya kutembelea na kukaa kwa mapumziko, sambamba na kuweka mahitaji muhimu ya wageni wetu na familia zao”.
Watu waliotembelea ukanda wa kijani wamesema kuwa, hakika Atabatu Abbasiyya imeandaa sehemu nzuri sana kwa mapumziko ya watu wa Karbala, tunaomba mradi huu udumu kwani eneo hili lipo mbali na msongamano wa watu wa mjini.