Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya amekutana na vitengo vitakavyo shiriki kwenye wiki ya Imamu.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Aalu Dhiyaau-Dini amekutana na kamati za vitengo vitakavyo shiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa.

Wamefanya kikao mbele ya wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo na kamati tendaji za wiki ya Imamu kimataifa.

Mheshimiwa katibu mkuu amehimiza kukamilisha maandalizi ya siku ya ufunguzi, akasisitiza umuhimu wa kujiandaa vitengo vyote kwa ajili ya siku ya ufunguzi, aidha akawataka wasomi wanufaike na tafiti zilizopo.

Mkutano ukajadili shughuli za maandalizi na mazingira bora sambamba na kujali huduma za watafiti.

Atabatu Abbasiyya inafanya kongamano la wiki ya Imamu kimataifa kwa mara ya kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyo tengana), na anuani isemayo (Uimamu ni nidhamu ya Umma), kongamano litaanza tarehe 6 – 13/ Julai/ 2023m, watashiriki wasomi wa Dini na sekula kutoka ndani na nje ya tatifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: