Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa awamu ya kwanza.
Rais wa kitengo hicho Shekhe Ammaar Hilali amesema “Kitengo kimekamilisha maandalizi ya kushiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa, kimepewa jukumu la kuratibu kongamano la siku ya Imamu Swadiq na Kaadhim (a.s) pamoja na kuratibu kongamano la kielimu katika siku ya kwanza ya wiki ya Imamu”.
Akaongeza kuwa “Tafiti zitakazo wasilishwa kwenye kongamano hilo zimefanyiwa mchujo, jumla zilikuwa tafiti 43, zimechujwa na kubaki tafiti 33”, akasema “Tafiti 14 zitawasilishwa kwa muda wa siku saba, kila siku zitawasilishwa tafiti mbili, moja asubuhi na nyingine jioni, tafiti zilizo baki zitaandikwa kwenye vitabu maalum vitakavyo tolewa wakati wa wiki ya Imamu”.
Akaendelea kusema “Kongamano litakuwa na mada tofauti zilizogawika kwenye makundi Matano, kutakuwa na mada zinazohusu Qur’ani, Hadithi, Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Historia”.
Kongamano la wiki ya Imamu linafanywa kwa mara ya kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).