Idara ya usalama katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha semina ya mbinu za kupambana na moto kwa wafanyakazi wa Ataba tukufu.
Mkufunzi wa semina hiyo kutoka idara ya usalama Sayyid Bilali Jabaar amesema “Idara ya usalama chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya imekamilisha semina ya mbinu za kupambana na moto kwa wafanyakazi wa Ataba tukufu”.
Akaongeza kuwa “Semina imejikita katika kuelezea vifaa vya kuzimia moto kwa kutumia mikono na namna ya matumizi yake pamoja na kuhakikisha usalama na mtu anayezima moto”.
Akaendelea kusema “Wanasemina wamefundishwa mbinu mbalimbali za kuzima moto kwa ustadi mkubwa”.