Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kupitia kituo cha taaluma za namba kimefanya makubaliano ya kushirikiana na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.
Mkuu wa kituo Sayyid Ammaar Jawadi amesema “Wageni wamejadili namna ya kushirikiana kielimu, kikao hicho kimehudhuriwa na Dokta Lubna Khamisi Mahadi kiongozi wa idara ya tafiti na uboreshaji, na Dokta Sinani Husam, mkuu wa kitengo cha miradi ya kimkakati katika uwanja wa tafiti na uboreshaji”.
Akaongeza kuwa “Kiongozi mkuu wa idara ya tafiti na uboreshaji ameonyesha utayali wa kushirikiana na kituo cha taaluma za namba katika ofisi ya Ataba tukufu, kwa lengo la kutoa huduma bora zaidi kwa taasisi za kielimu za Iraq”.
Katika kikao hicho wamejadili kuhusu utaratibu wa kutoa huduma na msaada kwa vyuo vikuu vya Iraq.