Kamati kuu inayosimamia wiki ya Imamu kimatifa, imefanya kikao cha kujadili ratiba ya wiki ya Imamu.
Kiongozi wa idara ya mawasiliano ya vyuo na shule Sayyid Maahir Khalid amesema “Kikao cha mwisho kimehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi na Sayyid Jawadi Hasanawi, pamoja na wasimamizi wa baadhi ya vitengo na wajumbe wa wiki ya Imamu, katika kikao hicho imejadiliwa ratiba ya wiki ya Imamu kimataifa kwa ujumla”.
Akaongeza kuwa “Katika kikao hicho umepangwa utaratibu wa mawasiliano, sehemu watakazo kaa washiriki, chakula, usafiri, sehemu maalum za kuongea na waandishi wa Habari na kutoa muongozo kwa watafiti”.
Akaendelea kusema “Kamati ya maandalizi imeandaa mkalimani maalum wa wageni watakaokuja kushiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa kutoka nje yaIraq”.
Atabatu Abbasiyya inafanya kongamano la wiki ya Imamu kimataifa mwaka huu kuanzia tarehe sita mwezi wa saba, chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyo tofautiana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).