Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amesema kuwa, wiki ya Imamu ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya Idul-Ghadiir na kuingiza tafiti katika maktaba za kiislamu.
Ameyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye ufunguzi wa wiki ya Imamu, iliyoratibiwa na kusimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotengana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).
Sayyid Swafi amesema kuwa “Maamuzi ya kuadhimisha wiki ya Imamu yamefikiwa baada ya kutafakari kwa kina kuwa tukio la Idul-Ghadiir msingi wake ni Imamu Ali (a.s), jambo hilo ni sehemu ya itikadi muhimu kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s)” akasisitiza kuwa “Wiki ya Imamu ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya Idhul-Ghadiir na kuingiza tafiti kwenye maktaba za kiislamu”.
Akaongeza kuwa “Lazima tutambue kuwa Mtume hateuliwi na watu, bali huteuliwa na Mwenyezi Mungu naye ni sawa na balozi wa Mwenyezi Mungu na kiunganishi baina ya walimwengu na muumba wao, hali kadhalika Uimamu”.
Akaendelea kusema “Madrasa ya Ahlulbait (a.s) kitu kitukufu zaidi kwao ni Qur’ani na Mtume Muhammad (s.a.w.w), wakituamrisha kitu lazima tufate, historia imeeleza wazi namna Mtume (s.a.w.w) alivyomjali Imamu Ali (a.s), bali Imamu Ali (a.s) ndiye msadikishaji aliyesadikishwa, Mtume Muhammad (s.a.w.w) alikuwa anaeleza ukaribu wake kwake, na miongoni mwa vielelezo ni tukio la Ghadiir, tunapoadhimisha tukio hilo tunaadhimisha jambo kubwa”.
Akaendelea kusema: “Siku ya Ghadiir inaonyesha Uimamu na utukufu wake, ni msingi wa kutawazwa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), kama alivyosikika Mtume (s.a.w.w) akiongea kuhusu kiongozi wa waumini, hivyo hivyo kwa Maimamu wengine, tukirejea katika asili lazima tutapata matokeo sawa. Namaanisha kuwa Mtume ndio msingi mtakatifu, naye kaeleza kuhusu msingi mwingine wa Uimamu, na msingi wa Maimamu ni kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twali (a.s)”.
Akafafanua kuwa “Jumla ya tafiti zilizotumwa kwa ajili ya kushiriki kwenye kongamano la wiki ya Imamu kimataifa awamu ya kwanza ni 240, zikachujwa hadi zikabaki 151, idadi ya nchi zinazoshiriki zipo 17”.