Katika siku ya kwanza.. Ufunguzi wa maonyesho kwa washiriki wa wiki ya Imamu.

Siku ya kwanza ya wiki ya Imamu imeshuhudia ufunguzi wa maonyesho kwa washiriki.

Atabatu Abbasiyya inasimamia shughuli za wiki ya Imamu chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).

Maonyesho yamefanywa kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, yamepambwa na mashindano ya uchoraji, hati za kiarabu, picha, jumla ya kazi mia moja na hamsini zimeshiriki.

Wiki ya Imamu inamashindano saba ya kitamaduni na kiufundi, nayo ni (Shindano la filamu fupi, shindano la kazi za mikono, shindano la mashairi, shindano la hati, shindano la adabu, shindano la video fupi, shindano la visa vifupi.

Wiki ya Imamu inafanyika tarehe 6 – 13/ Julai/ 2023, mada zaidi ya thelathini zitawasilishwa, miongoni mwa mada hizo ni (Qur’ani, Hadithi, Aqida, Fiqhi, Usulu, Siasa, Jamii, Malezi, Saikolojia, Lugha, Adabu na Historia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: