Rais wa watalam wa picha katika nchi ya Lebanon Shekhe Ali Yasini Al-Aamiliy, amesema kuwa wiki ya Imamu inamanisha kuthibitisha itikadi ya kumtawalisha Imamu Ali (a.s).
Ameyasema hayo kwenye kikao cha ufunguzi wa wiki ya Imamu inayosimamiwa na Ataba tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotengana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).
Shekhe Al-Aamiliy ameviambia vyombo vya Habari kuwa “Wiki ya Imamu inamanisha kuthibitisha hadithi sahihi na itikadi ya kumtawalisha kiongozi wa waumini (a.s) jambo ambalo ndio sharti ya kutimia kwa uislamu na Imani”.
Akaongeza kuwa “Wiki ya Imamu inafundisha kufuata mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na kuwatambua”, akasisitiza kuwa “Kuwatii wao na kumtii Mtume (s.a.w.w) ni sawa na kumtii Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Wiki ya Imamu inafanyika tarehe 6 – 13/ Julai/ 2023, mada zaidi ya thelathini zitawasilishwa, miongoni mwa mada hizo ni (Qur’ani, Hadithi, Iqida, Fiqhi, Usulu, Siasa, Jamii, Malezi, Saikolojia, Lugha, Adabu, Historia).