Kuanza kwa vikao vya lugha ya Kiingereza katika ratiba ya wiki ya Imamu kimataifa.

Vikao vinavyo endeshwa kwa lugha ya kiingereza vimeanza leo jioni vikiwa na washiriki kutoka ndani na nje ya Iraq.

Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kongamano la wiki ya Imamu kimataifa chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).

Vikao vinavyo endeshwa kwa lugha ya kiingereza vimeanza Jumamosi asubuhi kwenye majengo ya shule za Al-Ameed, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya wiki ya Imamu awamu ya kwanza, vimepata washiriki wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

Kuna mada zaidi ya thelathini zinazo tarajiwa kuwasilishwa katika wiki ya Imamu, miongoni mwa mada hizo ni (Qur’ani, Hadithi, Aqida, Fiqhi, Usulu, Siyasa, Mambo ya kijamii, Malezi, Saikolojia, Lugha na Historia), pamoja na mada zinazohusu alama za kudhihiri.

Shughuli za wiki ya Imamu zimeanza jioni ya siku ya Alkhamisi tarehe 6 Julai 2023 na zitaendelea kwa muda wa siku saba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: