Kuanza kwa vikao vya siku ya tatu katika wiki ya Imamu kimataifa awamu ya kwanza.

Vikao vya siku ya tatu katika wiki ya Imamu kimataifa awamu ya kwanza vinafanyika katika chuo cha Al-Ameed, vikihutubiwa na wahadhiri kutoka ndani na nje ya Iraq.

Atabatu Abbasiyya inafanya maadhimisho ya wiki ya Imamu kimataifa kwa mara ya kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).

Vikao vya siku ya Jumamosi vimefanywa ndani ya chuo kikuu cha Al-Ameed, ikiwa ni siku ya tatu ya kongamano hilo, wameshiriki wahadhiri kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kuna mada zaidi ya thelathini zinazo tarajiwa kuwasilishwa katika wiki ya Imamu, miongoni mwa mada hizo ni (Qur’ani, Hadithi, Aqida, Fiqhi, Usulu, Siyasa, Mambo ya kijamii, Malezi, Saikolojia, Lugha na Historia).

Shughuli za kongamano zilianza asubuhi ya siku ya Alkhamisi, tarehe 6 Julai 2023m na zitaendelea kwa muda wa siku saba, katika siku hizo zinatarajiwa kuwasilishwa zaidi ya mada thelathini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: