Miongoni mwa shughuli za wiki ya Imamu awamu ya kwanza: Kukamilika kwa kikao cha jioni kilichokuwa na uwasilishaji wa dama kwa lugha ya kiingereza.

Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha vikao maalum vya jioni vilivyokuwa na uwasilishaji wa mada kwa lugha ya kiingereza, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya kwanza.

Asubuhi ya Jumamosi katika shule za Al-Ameed, kimefanywa kikao maalum kwa lugha ya kiingereza, kilicho hudhuriwa na wajumbe wengi kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kikao cha asubuhi kimeongozwa na Sayyid Haidari Ghazi, jumla ya mada saba zimewasilishwa huku kikao cha jioni kikijadili mada tato kutoka kwa wahadhiri wa ndani na nje ya Iraq, mwisho wa kikao wahadhiri wakapewa zawadi ya midani na vyeti vya ushiriki.

Vikao vya wiki ya Imamu vilianza asubuhi ya Alkhamisi tarehe 6 Julai 2023 na vinaendelea kwa muda wa siku saba, jumla ya mada zaidi ya thelathini zitawasilishwa, miongoni mwa mada hizo ni (Qur’ani, Hadithi, Aqida, Fiqhi, Usulu, Siasa, Jamii, Malezi, Lugha, Adabu na Historia) sambamba na mada zinazohusiana na alama za kudhihiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: