Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, ametoa nasaha kwa washiriki wa kongamano la wiki ya Imamu kimataifa linalosimamiwa na Ataba tukufu.
Ametoa nasaha hizo wakati akichangia mada ya siku ya tatu iliyopewa jina la (Sajjaad na Baaqir (a.s) ni taa mbili zinazoangaza).
Sayyid Swafi amepongeza juhudi za wahadhiri wa kongamano, hakika wameonyesha picha halisi ya maudhui ya Uimamu, akasema kuwa utafiti unaosomwa ni tofauti na ulioandikwa, mtafiti hutumia muda mrefu kuandika anayoyaona sahihi.
Akaongeza kuwa, kuna tofauti ya mfumo wa kuandika na mfumo wa kuongea, mhadhiri anatakiwa kutuliza hadhira yake kwa kutumia mahadhi na sauti yake, kwa kuongea mambo sahihi sambamba na ukubwa wa sauti yake kulingana na mada anayowasilisha.
Sayyid Swafi akasisitiza kuwa, mada zote zilizowasilishwa kuhusu Imamu Sajjaad na Baaqir (a.s) ni nzuri.
Akapendekeza kuwa, maoni yaliyotolewa yaandikwe pembezoni mwa mada husika, ili msomaji atambue kilicho jiri wakati wa vikao, na muwasilishaji aweze kunufaika na maoni hayo baadae, akasema kuwa anategemea swala hili litaendelea katika miaka ijayo.