Kikao cha jioni katika siku ya tatu ya wiki ya Imamu awamu ya kwanza ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) kwa ushiriki wa wasomi kutoka ndani na nje ya Iraq.
Atabatu Abbasiyya inafanya kongamano la Imamu kimataifa awamu ya kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Uimamu ni mfumo wa umma).
Kikao kilianza asubuhi ya siku ya Jumapili ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya siku ya tatu katika wiki ya Imamu kimataifa, kikao hicho kimehudhuriwa na watu wengi kutoka nje na ndani ya Iraq.
Siku ya tatu imepewa kauli mbiu isemayo “Sajjaad na Baaqir (a.s) ni taa mbili zinazo angaza”, kikao kimesimamiwa na kitengo cha Habari na utamaduni, kituo cha Swadiqaini, kituo cha Shekhe Tusi na Jumuiya ya Al-Ameed.
Wiki ya Imamu inadumu kwa muda wa siku saba, mada zaidi ya thelathini zinawasilishwa, miongoni mwa mada hizo ni (Qur’ani, Hadithi, Aqida, Fiqhi, Siasa, Jamii, Malezi, Lugha, Adabu na Historia), bila kusahau mambo yanayohusiana na alama za kudhihiri.