Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kumbukizi ya Muhadhiri wa mimbari ya Husseini Shekhe Muhammad Baaqir Almaqdasi.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, umefanya majlisi ya kumbukizi ya Muhadhiri wa mimbari ya Husseini Dokta Muhammad Baaqir Almaqdasi.

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu Sayyid Jawadi Hasanawi na baadhi ya watumishi wa Ataba tukufu.

Atabatu Abbasiyya imeshindikiza muili wa Muhadhiri wa Husseini mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) Ijumaa ya tarehe 7/7/2023 kabla ya kwenda kumzika katika mji wa Najafu.

Shekhe Maqdasi ni miongoni mwa wahadhiri wakubwa, alizaliwa katika mji wa Najafu mwaka 1939m, akajiunga na Hauza mwaka 1958, akaendelea kufungamana na Hauza maisha yake yote, alianza kuwa Muhadhiri akiwa na miaka 19, sehemu zingine alizoenda kusoma ni Basra, Kuwait, Baharain, Qatar, Maskat, Falme za kiarabu, Lebanon na Landan, akapata udaktari wa elimu ya kiislamu katika chuo kikuu cha kimataifa katika jiji la Landan.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: