Msomaji kutoka Majmaa-Ilmi ameshinda nafasi ya pili kwenye shindano ya Ghadiir ya kuadhini.

Msomaji wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Ridhwa Zubaidi amekuwa mshindi wa pili kwenye mashindano ya Ghadiir ya kutoa adhana.

Shindano hilo limefanywa katika msikiti wa Kufa, lilikuwa na washindani 50 limesimamiwa na uongozi wa msikiti wa Kufa na Mazaru zilizo chini yake.

Alama za mshindi wa kwanza na wa pili zimekaribiana sana, Zubaidi amepata alama 90 na robo huku mshindi wa kwanza akiwa na alama 90 na nusu.

Kamati ya majaji imesema kuwa Zubaidi anatamka kwa ufasaha mkubwa wito wa swala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: