Msomaji wa Atabatu Alawiyya Sayyid Hani Mussawi ameshiriki kwenye kikao hicho, pamoja na msomaji wa Ataba mbili bwana Osama Karbalai, msomaji wa Atabatu Radhawiyya Muhammad Jawaad Banahi na usomaji wa kikundi.
Kikao hicho kimesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa.
Usomaji wa Qur’ani ni sehemu ya ratiba ya wiki ya Imamu, wasomaji wa Qur’ani kutoka ndani na nje ya nchi wameshiriki, jambo hilo linaonyesha namna Atabatu Abbasiyya inavyojali swala la Qur’ani ambayo ni muhimu sana katika mada ya Utume na Uimamu kwani ndio vizito viwili visivyotengana.
Kikao cha usomaji wa Qur’ani kilichofanywa ndani ya haram tukufu ya Abbasi, kimehudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru.