Sayyid Swafi ameelekeza kutafsiri mada zilizo wasilishwa kwenye wiki ya Imamu kimataifa katika lugha ya kiingereza na kuzisambaza.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ameelekeza kutafsiri mada zilizo wasilishwa kwenye wiki ya Imamu katika lugha za kigeni na kuzisambaza.

Ameyasema hayo alipokutana na wahadhiri wa kigeni walioshiriki kongamano hilo.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya wiki ya Imamu kimataifa Dokta Haidari Mussawi amesema “Muheshimiwa Sayyid Swafi Ameelekeza kuongeza idadi za mada, kwa kualika wahadhiri wa kigeni kwenye makongamano yanayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, hususan kongamano la wiki ya Imamu”, aidha ameelekeza kutafsiri mada zilizo wasilishwa kwenye kongamano la wiki ya Imamu kimataifa awamu ya kwanza katika lugha zingine na kuzisambaza.

Akaongeza kuwa “Muheshimiwa amehimiza kuweka maudhui zinazofahamika na kuendana na malengo ya Atabatu Abbasiyya, na kujiepusha na kila jambo linaloweza kuleta utata”.

Naye mkufunzi wa chuo kikuu Dokta Hassan Shaikhah amesema “Kikao tulichofanya na Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kinaonyesha namna anavyojali wiki ya Imamu, tumeongea nukta nyingi muhimu kuhusu Ahlulbait (a.s) na ulazima wa kuhubiri amani na maelewano kila sehemu ya dunia”.

Rais wa jarida la (Hindu wa leo) Dokta Azishan Abbasi amesema “Kutokana na mazungumzo yetu na Sayyid Swafi tunategemea mada zilizo wasilishwa kwenye wiki ya Imamu kimataifa zitasambazwa dunia nzima hususa kwa waislamu wa nchi ya India”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: