Rais wa muungano wa vyuo vikuu vya kiarabu amekipongeza chuo kikuu cha Al-Ameed kwa mafanikio yake kielimu.

Rais wa muungano wa vyuo vikuu vya kiarabu Dokta Amru Izat Salama, amepongeza maendelea ya chuo kikuu cha Al-Ameed kielimu.

Ameyasema hayo wakati wajumbe wa muungano wa vyuo vikuu vya kiarabu wakiongozwa na katibu mkuu, rais wa chuo kikuu cha Furatu Ausat na rais wa chuo kikuu cha Karbala, walipo tembelea chuo kikuu cha Al-Ameed.

Akasisitiza kuwa “Chuo kikuu cha Al-Ameed kimepata maendeleo makubwa katika sekta ya elimu kitaifa na kimataifa, kimekuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti za kielimu.

Ugeni huo umepokewa na mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya, Dokta Afdhalu Shami na baadhi ya viongozi wa chuo.

Wamejadili namna ya kuboresha ushirikiano na kubadilishana uzowefu wa kielimu, aidha kulinda ubora wake kwa kushirikiana na taasisi zilizopo kwenye muungano huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: